Gadget
| This content isn't available over encrypted connections yet. |
THURSDAY, AUGUST 18, 2016
WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA BALOZI WA ISRAEL NCHINI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Israel Nchini Tanzania Mh. Yahel Vilan alimpomtembelea Ofisini kwake barabara ya Luthuli jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akijadiliana jambo na Balozi wa Israel Nchini Tanzania Mh Yahel Vilan alimpomtembelea Ofisini kwake barabara ya Luthuli jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni Maafisa toka Wizara ya mambo ya nje waliongozana na Balozi huyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akisoma Nakala za machapisho alizopatiwa na Balozi wa Israel Nchini Tanzania Mh . Yahel Vilan.
THURSDAY, AUGUST 18, 2016
VIJANA ELFU 18 KUSOMA UFUNDI STADI KWA SIMU KUPITIA AIRTEL FURSA VSOMO
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na VETA imeingia mkoani Arusha kuendelea kutoa uelewa kwa vijana kukamata FURSA na kusomo kozi mbalimbali toka VETA kupitia mfumo wao wa simu ujulikanao kama VSOMO. hadi sasa zaidi ya vijana elfu kumi na nane nchini wamejisajili kusoma kwa mfumo huo wa simu za mkononi huku mikakati yao ikiwa ni kuongeza kozi 10 zaidi ili wanafunzi kuendelea kujisomea.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mauzo kanda ya kaskazini Bw, Brighton Majwala wakati alipoongea na wajasiliamali na madereva bodaboda waliokusanyika stand kuu Arusha jana,
“Airtel na Mamlaka ya ufundi stadi VETA lengo letu ni kuwafikishia elimu ya ufundi vijana wengi nchini, upande wetu Airtel tunahakiksha mtandao upo vyema ili vijana waweze kusoma bila kukwama, hadi leo hii tayari vijana zaidi ya milioni 18 wameshakamata FURSA hii kwa kupakua aplikesheni au mfumo huu wa VSOMO katika simu zao” alieleza Bw Majwala
Majwala aliendelea kusema kuwa “mpango wetu Airtel na VETA ni kuongeza uelewa kwa vijana ili wasome kozi zilizopo sasa ikiwemo ya ufundi piki piki, umeme wa nyumbani, ufundu simu, ufundi wa aluminium, utaalam wa masuala ya urembo, pamoja na ufundi wa kuchomea vyuma”.
kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel alisema “kutokana na VSOMO kuwa na idadi kubwa ya vijana waliojisajili tayari Airtel kwa kushirikiana na wadau wetu VETA tuko katika utekelezaji wa kuongeza kozi zingine zaidi ya kumi ili kuongeza wigo wa kuchagua pamoja na kuongeza idadi ya wanaosoma na kuhitimu”. alieleza mmbando
“tunampango wa kuongeza kozi zingine 10 kabla ya mwezi wa 12 ambapo sasa hivi tayari VETA wako katika utaratibu wa kuzifanyia kazi kozi hizo ili ziweze kuingia katika mtandao” alisema Mmbando
“Mradi wa VSOMO ni sehemu ya mpango wa Airtel FURSA wenye lengo la kuwawezesha vijana pamoja na kutimiza kauli mbiu ya “Airtel the smartphone network” kwa kujipatia elimu ya ufundi stadi toka VETA kwa smartphone zao” alisisitiza Mmbando
Airtel kwa kushirikiana na VETA nchini ilizindua mfumo wa masomo ya ufundi stadi kwa njia ya mtandao VSOMO mwezi Julai 2016 ambapo mpaka sasa tayari mfumo huu umetambulishwa katika mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Arusha, Morogoro na Mwanza lakini kutokana na uhitaji mkubwa kwa vijana tayari mfumo huo umepokea maombi ya vijana toka mikoa 25 kwa kupakua mfumo/aplikesheni hiyo hiyo na kuomba kusoma kwa njia ya simu za Airtel.
Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando (katikati) akitoa maelekezo kwa baadhi ya wanaotoa huduma ya usafiri wa Boda boda Arusha eneo la stand kuu Arusha jinsi wanavyoweza kujiunga na mfumo wa VSOMO na kusoma masomo ya Ufundi stadi kupitia mtandao wa Airte jana.
Mkuu wa mauzo wa Airtel kanda ya kaskazini Bw, Bryton Majwala na wafanyakazi wengine wa Airtel kwa pamoja wakizungumza na baadhi ya wajasiliamali na watoa huduma ya usafiri wa Boda boda Arusha eneo la stand kuu Arusha jinsi wanavyoweza kujiunga na mfumo wa VSOMO na kusoma masomo ya Ufundi stadi kupitia mtandao wa Airtel jana.
Mkuu wa mauzo wa Airtel kanda ya kaskazini Bw, Bryton Majwala akitoa maelekezo kwa baadhi ya wajasiliamali wanaotoa huduma ya usafiri wa Boda boda Arusha eneo la stand kuu Arusha jinsi wanavyoweza kujiunga na mfumo wa VSOMO na kusoma masomo ya Ufundi stadi kupitia mtandao wa Airtel mkoani jana.
THURSDAY, AUGUST 18, 2016
MGODI WA DHAHABU WA BULYANHULU WATENGENEZA AJIRA KWA WAJASILIAMALI VIJIJINI KUPITIA MRADI WA MADAWATI
THURSDAY, AUGUST 18, 2016
DC KASESELA AKUTANA NA MASELA WA KIHESA, MJINI IRINGA, APIGA JALAMBA NA MGAMBO
Katika kupunguza kasi ya uhalifu na kuwawezesha Vijana wa Iringa, Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alikutana na vijana wa kijiwe cha Kihesa, ambao wengi wao wanajishughulisha na kuosha magari na kuwaomba kusaidiana naye katika kutokomeza udokozi.
Vijana hao walimuomba Mkuu wa Wilaya awasaidie upatikanaji wa mashine ya kuoshea magari ambayo aliwahidi kuwatafutia ndani ya siku 2 ili mradi wajiunge kwenye kikundi na wafungue akaunti benki. Vijana hao walimsukuru sana mkuu wa wilaya na kuahidi kuwa watiifu wa sheria na kuchapa kazi. Kikundi hicho kina vijana 25.
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akifanya mazungumzo na Kikundi cha vijana 25 wanaojishughulisha na uoshaji wa magari katika eneo la Kihesa, Mjini Iringa.
Kasesela akipitia taarifa ya Kikundi hicho aliyokabidhiwa.
Akitoka eneo hilo baada ya kumaliza kuzungumza na vijana hao.
THURSDAY, AUGUST 18, 2016
IGP MANGU AWAAGA ASKARI 14 WA KIKOSI MAALUM CHA POLISI (S.F.U)
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akimuuaga PC Prosper Yenda yenda wa kikosi maalum cha Jeshi la Polisi ( S.F.U) ambaye ni miongoni mwa askari 14 wanaokwenda nchini Jordan kwa kozi maalum ya kupambana na uhalifu na wahalifu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akiwa katika picha ya pamoja na askari 14 wa kikosi maalum cha Jeshi la Polisi (S.F.U) ambao wanaokwenda nchini Jordan kwa kozi maalum ya kupambana na uhalifu na wahalifu. (Picha na Tamimu Adam- Jeshi la Polisi).
THURSDAY, AUGUST 18, 2016
WAZIRI MKUU AWAWEKA SAWA WATUMISHI WA OFISI YAKE, TAYARI KWA SAFARI YA DODOMA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema safari ya kuhamia Dodoma imeiva na amewataka watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wajipange kisaikolojia.
Ametoa kauli hiyo jana (Jumatano, Agosti 18, 2016) alipokutana na kuzungumza na watumishi wa ofisi yake kutoka taasisi, idara na vitengo mbalimbali waliopo Dar es Salaam.
Waziri Mkuu aliwataka watumishi hao watambue kuwa uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao chimbuko lake ni agizo lililotolewa Oktoba Mosi, 1973 kwenye Mkutano Mkuu wa 16 wa chama cha TANU.
“Tangu wakati huo kumekuwa na juhudi mbalimbali zilizofanyika ili kuandaa miundombinu na hata awamu ya nne ilisimamia kwa kiwango kikubwa uwekaji wa miundombinu hiyo,” alisema.
“Pia tukumbuke kauli ya Mheshimiwa Rais aliyotoa kwenye hotuba yake ya Julai 23, 2016 alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM, na akairudia tena Julai 25, kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa na mimi siku hiyo hiyo nikaweka msisitizo,” alisema.
“Napenda kuwatoa hofu, mambo yanaenda vizuri ila mtambue kuwa safari imeiva sasa. Kikubwa ni kwamba tutakwenda kwa awamu kama ambavyo imepangwa,” alisema.
Aliwataka watumishi hao wazidishe mshikamano miongoni mwao huku wakitambua kuwa wana dhamana ya kuwatumikia Watanzania kwa uadilifu na uaminifu. “Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu tunapaswa tutambue dhamana tuliyonayo. Tufanye kazi kwa bidii. Tuhakikishe kila kilichopangwa kinafanyika kwa ufanisi na kinafanikiwa,” alisema.
THURSDAY, AUGUST 18, 2016
JWTZ YANYAKUA VIKOMBE VITATU MASHINDANO YA MAJESHI MJINI KIGALI
Mnadhimu mkuu wa Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania Luteni Generali Venance mabeyo akisalimiana na wachezaji wa timu ya Soka ya Tanzania wakati wa mchezo wa mwisho dhidi ya Rwanda Tanzania ilifungwa bao 1-0 na kushika nafasi ya tatu
Mwanariadha Siata Kalinga akipokea kikombe cha mshindi wa tatu kwa riadha wanawake kutoka kwa Naibu Mkuu wa Majeshi wa Uganda Luteni Jenerali Charles Angina.
Viongozi waandamizi wa majeshi waliowakilisha wakati wa sherehe za kufungwa mashindano ya Majeshi kwa nchi za Afrika Mashariki, yaliyokuwa yakifanyika Mjini Kigali nchini Rwanda kutoka kulia ni mkuu wa majeshi wa Rwanda Jenerali Patrick Nyamvumba, akifuatiwa na Mkuu wa majeshi wa Kenya Jenerali Samson Mwathethe, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Venance Mabeyo pamoja na Naibu Mkuu wa Majeshi wa Uganda Luteni Jenerali Charles Angina. (picha na Selemani Semunyu)
THURSDAY, AUGUST 18, 2016
BENKI YA DUNIA KUENDELEA KUIPIGA TAFU SEKTA YA MAJI NCHINI
KATIKA kuhakikisha sekta ya Maji inakua kwa kasi na inatosheleza mahitaji ya sasa ya huduma ya maji, Benki ya Dunia imejitolea kulisaidia Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO), ili kusaidia katika upatikanaji wa huduma ya Majisafi na Majitaka katika maeneo mbalimbali ya wakazi wa jiji la Dar es salaam pamoja na Miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.
Hayo yamezungumzwa na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini, Bi. Bella Bird, ambaye alikuwa ameambatana na wajumbe wake katika kikao cha pamoja na Waziri wa Maji, Mhandisi Gerson Lwenge, pamoja na Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO). Kikao ambacho kililenga uboreshaji na upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo kadhaa ya jijini Dar es Salaam hasa maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo.
Aidha, Mwakilishi huyo wa Benki ya Dunia, ameridhishwa na juhudi za makusudi zinazofanywa na Dawasco katika kuwapatia wananchi huduma ya Majisafi, pamoja na kupambana na kiwango cha Maji kinachopotea bila sababu ya msingi.
Ameeleza kuwa Benki ya dunia imetenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Majisafi na Majitaka ili kuimarisha uendeshaji wa utoaji wa huduma ya Maji kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kutekeleza kikamilifu kampeni ya “Mama Tua Ndoo Kichwani” ili kuwapunguzia akina mama wengi tatizo la Maji, kwani ndio wanaoonekana kuwa wahanga wakuu wa tatizo hilo.
“Nimeridhishwa na utendaji wenu wa kazi, jinsi ambavyo mmejipanga katika kufanya kazi, hasa juhudi zenu mnazoziweka katika kupambana na upotevu wa Maji na kuwapatia wananchi huduma ya Maji” alisema Bi. Bird
Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja ameishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano mzuri waliouonesha, na kwamba kiasi cha fedha kilichotengwa na Benki ya Dunia kitatumika katika kuboresha na kutatua changamoto mbalimbali zinazolikabili shirika katika utoaji wa huduma ya Maji. “Changamoto ni nyingi katika utoaji wa huduma ya Maji, naamini kuwa kiasi cha fedha kilichotengwa kitasaidia kuondoa changamoto hizo” alisema Mhandisi Luhemeja.
Benki ya dunia imekuwa ikifadhili miradi mingi ya maendeleo hapa nchini ikiwamo miradi mbalimbali katika sekta ya Maji, Nishati na Madini, Kilimo na Mifugo, pamoja na Uchumi na Biashara.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akifungua kikao cha pamoja na ujumbe wa Benki ya dunia, Wizara ya Maji ,Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (Dawasco ) na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (Dawasa) namna ya kutatua changamoto za usambaza Maji kwenye Jiji la Dar es Salaam yakiwamo Mivujo na Miundombinu chavu , kilichofanyika Jijini Dar es salaam mapema wiki hii.
THURSDAY, AUGUST 18, 2016
WANAFUNZI HEWA 2331 KATIKA SHULE ZA SEKONDARI MKOANI SIMIYU WABAINIKA
Baada ya kufanya uhakiki wa Wanafunzi Uongozi wa Mkoa wa Simiyu umebaini uwepo wa wanafunzi hewa 2331 katika shule za Sekondari za Mkoa huo.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka wakati alipozungumza na Walimu Wakuu na Waratibu Elimu Kata mara baada ya kuwakabidhi Vishikwambi (Tablets) vilivyotolewa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la EQUIP Tanzania kwa ajili ya utunzaji wa Takwimu muhimu za Sekta ya Elimu,.
Mtaka amesema kati ya Halmashauri sita za Mkoa huo, Ni Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi tu ambayo haina wanafunzi hewa wakati Halmashauri ya Wilaya ya Busega ikiwa na wanafunzi hewa 110, Itilima 2137, Maswa 14, Meatu 125 na Halmashauri ya Mji wa Bariadi 439.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungmza na Walimu wakuu na Waratibu wa Elimu wa Kata baada ya kuwakabidhi Vishikwambi vilivyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la EQUIP Tanzania, kwa ajili ya kutunza kumbukumbu na tawimu sahihi za masuala ya elimu.
Kufuatia kuwepo kwa wanafunzi hewa Mkuu wa Mkoa huo amesema, Serikali Mkoani humo imepanga kufanya mabadiliko ya Wakuu wa Shule za Sekondari katika Mkoa mzima, wakati taratibu za kinidhamu zikiendelea kwa wakuu wa shule waliotoa takwimu za uongo za wanafunzi katika shule zao, wakati kwa upande wa shule za Msingi, mabadiliko yatafanyika baada ya kumaliza mtihani wa darasa la saba.
Mtaka amesema kabla ya uteuzi wa wakuu wa shule na walimu wakuu utafanyika upekuzi (vetting) kwa wale watakaopendekezwa ili kujiridhisha kama wahusika wana sifa na uwezo wa kuendesha shule na kusimamia fedha za Serikali zinazopelekwa shuleni kwa ajili ya kugharama elimu ya bila malipo.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini (kushoto) akizungumza na Walimu wakuu na Waratibu wa Elimu wa Kata baada ya kukabidhiwa Vishikwambi na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (katikati)vilivyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la EQUIP Tanzania, kwa ajili ya kutunza kumbukumbu na tawimu sahihi za masuala ya elimu(kulia)ni Afisa Elimu Mkoa, Julius Nestory.
“ Serikali inaendelea kupelekea fedha moja kwa moja katika akaunti za shule, kwa hiyo mkuu wa shule au mwalimu mkuu ni afisa masuuli katika shule yake. Ipo haja kwa sisi kujiridhisha kama Serikali kuwa anayeteuliwa kushika nafasi ya kuongoza shule ana uwezo na sifa ya uadilifu. Sitakuwa tayari kuona katika mkoa huu kuna walimu wakuu wazoefu wa kula fedha za Serikali na wakaendelea kuongoza shule” alisema Mtaka.
Akitoa shukrani kwa Shirika la EQUIP Tanzania, Mkuu wa Mkoa amesema Shirika hilo limekuwa msaada katika kutatua baadhi ya changamoto za Watendaji katika Sekta ya Elimu mkoani Simiyu ikwa ni pamoja na kuwawezesha Waratibu Elimu Kata kwa kuwapa pikipiki na kuwapa fedha za mafuta shilingi 206,000 kwa kila mwezi pamoja na kutoa mafunzo kwa walimu wakuu na walimu wakuu wasaidizi.
Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa (kushoto) akipokea Vishikwambi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka(kulia) kwa ajili ya Walimu Wakuu na Waratibu Elimu Kata wa Halmashauri hiyo.
Aidha, Mtaka amesema analishukuru shirika hilo kuona umuhimu wa kutoa vishikwambi kwa Walimu wakuu na Waratibu Elimu Kata ambavyo ameelekeza vitumike kutunza takwimu sahihi za kieleimu ikiwemo idadi ya walimu na wanafunzi.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini amewataka Walimu Wakuu na Waratibu Elimu Kata kuvitunza vishikwambi hivyo na kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Nelasi Mulungu(kushoto) akipokea Vishikwambi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka(kulia) kwa ajili ya Walimu Wakuu na Waratibu Elimu Kata wa Halmasahuri hiyo.
Naye Mkuu wa EQUIP Tanzania Mkoa wa Simiyu, Phoebe Okeyo amesema Vishikwambi hivyo vitawasaidia Viongozi wa Elimu ngazi ya Mkoa, Wilaya na kata kupata taarifa za masuala mbalimbali yanayofanyika shuleni.
“Sasa hivi mtegemee kupata taarifa sahihi katika sekta ya Elimu kwa sababu ya hivi vifaa tulivyovitoa leo, tumeanza kama pilot study kwa Mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Mara, Tabora, Dodoma,Lindi na Kigoma. Tunatarajia kuongeza mikoa ya Katavi na Singida Januari, 2017” alisema Okeyo.
Jumla ya Vishikwambi(tablets) 637 vimetolewa kwa Walimu wakuu 516 na Waratibu Elimu Kata 121 kutoka Halmashauri zote sita za Mkoa wa Simiyu, ambapo kila kimoja kina thamani ya shilingi 315,000/=.
Baadhi ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu Kata wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (hayupo pichani) mara baada ya kukabidhiwa Vishikwambi vilivyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la EQUIP Tanzania, kwa ajili ya kutunza kumbukumbu na tawimu sahihi za masuala ya elimu.
THURSDAY, AUGUST 18, 2016
KUTOKA MAKTABA YA GLOBU YA JAMII: HAWA NDIO WAZEE WALIOANZISHA VUGUVUGU LA KUSAKA UHURU WA NCHI YETU
Kutoka kulia waliosimama. 1. Abdallah Shomari (Tandamti no. 3 )2. Nassoro kalumbanya (simba str.) 3. Said Chamwenyewe (Aggrey/Congo str.) 4. Mtoro Ally (Muhonda str.) 5. John Rupia (Misheni kota) 6. Julius Nyerere( Pugu Sekondari ) 7. Said Chaurembo (Congo/ Mkunguni str.) 8. Jumbe Tambaza( Upanga ) 9. Sheikh Suleiman Takadir (Mafia /Swahili) 10. Dossa Aziz ( Mbaruku /Somali kipande ) 11. Mshume Kiyate (Tandamti) 12. Juma Sultan (Kitchwele karibu na kanisa dogo ) 13. Maalim Shubeti (Masasi/ Likoma) 14. Rajab Simba ( kiungani str.) 15. Waziri Mtonga (Kilosa no. 18 , Ilala) 16. Mwinjuma Mwinyikambi ( Mwananyamala) 17. Maxi Mbwana ( Aggrey /Kongo ) 18. Usia Omari (Sungwi ,Kisarawe) 19. Sheh Issa Nasir ( Bagamoyo)
THURSDAY, AUGUST 18, 2016
WILAYA YA PANGANI KUFANYWA YA MFANO KWA KUUNGANISHIWA UMEME YOTE
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mkaramo kilichopo wilayani Pangani mkoani Tanga. Waziri Muhongo yupo mkoani Tanga kwa ajili ya kukagua miradi ya kusambaza umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na kuzungumza na wananchi.
Na Greyson Mwase, Pangani
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa Serikali ina mpango wa kusambaza nishati ya umeme katika wilaya nzima ya Pangani na kuifanya kuwa wilaya ya mfano ndani ya kipindi cha miaka miwili.
Profesa Muhongo aliyasema hayo alipokuwa akihutubia katika kijiji cha Mkaramo kilichopo wilayani Pangani mkoani Tanga. Profesa Muhongo yupo mkoani Tanga kwa ajili ya kukagua miradi ya usambazaji wa umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Kabla ya kuwasili katika kijiji hicho msafara wa Profesa Muhongo ulisimamishwa na wananchi wa kijiji cha Sakura kilichopo wilayani Pangani mkoani Tanga waliokuwa na mabango wakiomba kupatiwa umeme katika kijiji chao.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mkaramo kilichopo wilayani Pangani mkoani Tanga (hawapo pichani).
Akizugumza kwa niaba ya wanakijiji wenzake, Boga Mbega alisema kuwa kijiji hicho kimekuwa gizani kwa muda wa miaka mingi hali inayopelekea uchumi katika kijiji hicho kudumaa.
Aliongeza kuwa kutokana na ukosefu wa umeme katika kijiji hicho wamekuwa wakifuata huduma za jamii kama vile matibabu na maji katika vijiji vya mbali na hivyo kuhisi kama wako kwenye kisiwa cha giza.
Mara baada ya Waziri Muhongo kuwasili katika kijiji cha Mkaramo na kuanza kuhutubia alisema kuwa kutokana na wilaya ya Pangani kuwa nyuma kimaendeleo kuliko wilaya nyingine nchini, Serikali imepanga mikakati ya kuhakikisha kuwa wilaya nzima ya Pangani pamoja na vijiji vyake vyote inapata nishati ya umeme ndani ya kipindi cha miaka miwili.
Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Zainab Abdallah Issa (kushoto) akiwasilisha mahitaji ya umeme katika wilaya ya Pangani.
Akielezea malengo ya kuipa kipaumbele wilaya ya Pangani kwenye mpango wa usambazaji wa umeme vijijini chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Profesa Muhongo alieleza kuwa ni kufuta umasikini kupitia uboreshaji wa huduma za jamii kama shule, zahanati, pamoja na kuzalisha ajira na kupunguza wimbi la vijana kukimbilia mjini kutafuta ajira.
Alisema katika utekelezaji wa mradi wa REA Awamu ya tatu katika wilaya ya Pangani, maeneo yatakayopewa kipaumbele cha kwanza ni pamoja na shule, zahanati, vyuo, makanisani na misikitini. Aliwataka wananchi wa wilaya ya Pangani kujiandaa na mradi huo kwa kubuni fursa mbalimbali kama vile kuanzisha vikundi vidogo vidogo kwa ajili ya kuanzisha viwanda, ukulima na ufugaji wa kisasa ili kujipatia maendeleo.
Waziri wa Nishati na Madini (kulia) akipokea kero mbalimbali kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Mkaramo.
Alifafanua kuwa ni wakati wa wakinamama wa wilaya ya Pangani kuachana na matumizi ya kuni na kutumia majiko ya umeme na gesi. Profesa Muhongo aliendelea kusema kuwa miradi ya umeme haihitaji siasa na kuwataka wananchi kuweka nguvu zaidi kwenye uchumi kwa kutumia nishati ya umeme badala ya kupoteza muda kwenye siasa.
Naye Mbunge wa Pangani Jumaa Hamidu Aweso (CCM) aliishukuru serikali kwa kuipa kipaumbele wilaya ya Pangani na kusisitiza kuwa wataanza kufanya uhamasishaji kwa wananchi wote wa Pangani . Aliwataka wananchi kuachana na maandamano ya siasa na badala yake waweke nguvu kwenye shughuli za kiuchumi zitakazowapatia maendeleo.
Alisema kuwa mara baada ya umeme katika wilaya nzima ya Pangani kupatikana, wawekezaji watajitokeza kuwekeza kwenye viwanda vya korosho na kuongezeka mapato katika halmashauri ya Pangani.
Wananchi wa kijiji cha Sakula kilichopo wilayani Pangani mkoani Tanga wakionyesha mabango yenye jumbe tofauti mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani) walipomsimamisha njiani kwa lengo la kuwasilisha kero mbalimbali wakati akielekea katika kijiji cha Mkaramo kwa ajili ya kuhutubia wananchi.
THURSDAY, AUGUST 18, 2016
BALOZI WA ISRAEL NCHINI AMTEMBELEA WAZIRI MAKAMBA.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea jambo na Balozi wa Israel Nchini Tanzania Mh. Yahel Vilan alimpomtembelea Waziri Makamba Ofisini kwake barabara ya Luthuli jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba wakijadiliana jambo na Balozi wa Israel Nchini Tanzania Mh Yahel Vilan alimpomtembelea Waziri Makamba Ofisini kwake barabara ya Luthuli jijini Dar es Salaam. Wengine ni Maafisa toka Wizara ya mambo ya nje waliongozana na Balozi huyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akisoma Nakala za machapisho alizopatiwa na Balozi wa Israel Nchini Tanzania Mh . Yahel Vilan.
THURSDAY, AUGUST 18, 2016
RAIS DKT MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKUU WA MKOA ARUSHA FELIX NTIBENDA,AMTEUA MRISHO GAMBO KUWA MKUU WA MKOA
Mkuu wa Mkoa mpya wa Arusha,Mrisho Gambo aliyeteuliwa na Rais,kuapishwa kesho ijumaa Ikulu jijini Dar
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya uongozi na kumteua Bw. Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia leo (Alhamisi, Agosti 18,2016).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Bw. Gambo anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Felix Kijiko Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Amesema Bw. Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha. Ataapishwa kesho (Ijumaa, Agosti 19, 2016) saa 3 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Bw. Gambo anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Felix Kijiko Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Amesema Bw. Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha. Ataapishwa kesho (Ijumaa, Agosti 19, 2016) saa 3 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,








No comments:
Post a Comment