There was an error in this gadget
FRIDAY, AUGUST 05, 2016
TPA YATAKIWA KUJENGA CHEREZO KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), kujenga chelezo (gereji ya kukarabati meli na vivuko), katika bandari ya Dar es Salaam ili kuokoa fedha nyingi zinazotumika kwa matengenezo nje ya nchi.
Waziri Prof. Mbarawa amesema hayo wilayani Kyela, wakati alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa meli mbili mpya za mizigo zinazojengwa na Kampuni ya Songoro Marine katika bandari ya Itungi ambayo ni Bandari Kuu katika Ziwa Nyasa na kuelezea kuridhishwa kwake na hatua za ujenzi uliofikiwa.
“Tukijenga chelezo Dar es Salaam tutaokoa fedha nyingi tunazozipeleka nje kila mwaka kwa ajili ya ukarabati wa vivuko na meli zetu", amesema Waziri Prof. Mbarawa. Amesisitiza kuwa kujengwa kwa chelezo katika bandari hiyo kutaongeza ajira kwa wananchi na pato kwa mamlaka kwani vyombo vya Sekta binafsi vitaweza kufanyiwa ukarabati wa vyombo vyao vya majini.
Aidha katika hatua nyingine, Waziri Mbarawa amekagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Kikusya-Ipinda- Matema KM 34.6 inayojengwa kwa kiwango cha lami na kumtaka Mkandarasi anayejenga barabara hiyo kukamilisha kwa viwango na ubora unaotakiwa ili idumu kwa muda mrefu.
"Tunapotoa fedha tumedhamiria kuhakikisha kitu tunachofanya kiendane na thamani ya fedha hiyo hivyo hakikisha unatekeleza kazi hii kwa kuzingatia viwango na ubora unaotakiwa",amesisitiza Prof.Mbarawa.
Hata hivyo Prof. Mbarawa amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa mkandarasi anayejenga barabara hiyo ili kuhakikisha kazi hiyo inakamilika kwa haraka na kufungua uchumi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Mbeya Eng. Paul Lyakurwa amemuomba Waziri Mbarawa kuruhusu wahandisi wazalendo kuendelea kusimamia mradi huo ikiwa ni hatua ya kuwajengea uwezo watanzania kusimamia miradi mikubwa nchini.
Waziri Prof. Mbarawa yupo katika ziara ya kukagua miundombinu na kuongea na wafanyakazi waliopo chini ya wizara yake katika mkoa wa Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akielekea katika Bandari ya Itungi kukagua maendeleo ya ujenzi wa meli mbili mpya zinazojengwa katika bandari hiyo wilayani Kyela.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Eng. Salehe Songoro akitoa maelezo ya hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa meli mbili mpya mbili kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, alipotembelea bandari ya Itungi kuona maendeleo ya ujenzi huo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Eng. Salehe Songoro wakati alipokagua moja ya mashine ya meli mpya inayojengwa katika bandari ya Itungi, wilayani Kyela.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akikagua risiti za malipo na Mhasibu wa Bandari ya Itungi (wa pili kushoto), wilayani Kyela.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
FRIDAY, AUGUST 05, 2016 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG ~ MTUMIE RAFIKI YAKO , MAONI: 0
FRIDAY, AUGUST 05, 2016
DTB RUNNING 70 YEARS ONLINE SOCIAL MEDIA CAMPAIGN
Diamond Trust Bank Tanzania (DTBT) is currently running an online social media campaign aimed at raising product awareness and rewarding its customers through online social media platforms.
The ongoing campaign, titled “70 Years – Count on us and Win!” allows customers, potential customers and stakeholders an opportunity to win daily prizes by answering trivial questions through the Bank’s Facebook pagewww.facebook.com/DTBTanzania.
Some notable prizes include customized soccer jerseys, cinema tickets, shopping vouchers, Samsung Galaxy J7 smartphones and a bumper prize of a MacBook air laptop.
The 70 years reflects on the Bank’s existence in Tanzania, thus being a commemoration of DTBT’s milestone achievements.
DTB Tanzania Head of Product Development & Marketing, Sylvester Bahati said the bank aim to be forefront in bringing services to their valued customers through all digital platforms.
"Our official Facebook page will help us communicate with our customers, potential customers and stakeholders about happenings in our communities and/or the latest activities and developments at the bank. We also want to be closer to our customers by offering them an interactive tool for effective customer service." He said.
Winner of Macbook of the DTB 70 Years Count on Us and Win" promotion, Evance Adelard receives his prize from the Diamond Trust Bank DTB Executive Director, Viju Cherian at an occasion held at the bank's Head Quarters in Dar es Salaam recently.
Diamond Trust Bank Tanzania Head of ICT Ms. Stella Masha (left) hands over prize jersey to one of the promotion winners of the “70 Years – Count on us and Win!” Mr. Said Mpanju from Kibaha at the short ceremony held in Dar es Salaam recently.
FRIDAY, AUGUST 05, 2016 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG ~ MTUMIE RAFIKI YAKO , MAONI: 0
FRIDAY, AUGUST 05, 2016
MSAADA TUTANI...JOHN MASHAKA YUKO WAPI ?
Ankal,
Ombi langu Ankal kwa leo ni kwamba, tumebakia kama mayatima kwa kutokuwepo kwa hawa magwiji na wataalamu wetu. John Mashaka, US Blogger , na Hildebrand Shayo Tunaomba re-union ya miaka kumi. Ndugu yetu John Mashaka atushushie nondo hata moja tu. Kwani mijadala yao ilikuwa ni kivutio kikubwa sana kwa wasomaji wa rika zote. Tunaobeba maboxi ughaibuni, stress zote za kazi ziliisha pale tulipoinamishwa vichwa vyetu kwenye computer kusoma mada za ndugu Mashaka na kisha majibu ya Gwiji US-Blogger.
Ankal, tukoshe roho japo kidogo. Tunaomba ile mijadala irudi hata kwa wiki moja tu, washabiki wa globu hatuna raha kabisa. Kama hataki kushiriki, basi atuandikie hata kibarua sisi wafuasi wake
Wake mtiifu, Mdau
Manchester, UK
FRIDAY, AUGUST 05, 2016 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG ~ MTUMIE RAFIKI YAKO , MAONI: 1
FRIDAY, AUGUST 05, 2016
YALE YALEEEEE... VIJIPU UPELE MBAGALA RANGITATU JIJINI DAR ES SALAAM
Wazee wa kijiweni katika eneo la Mbagala Rangi tatu jijini Dar es salaam wakipata kikombe cha kahawa huku pembezoni kukiwa na lundo la uchafu lililotolewa kwenye mtalo kama alivyokutwa na kamera ya Globu ya Jamii
Mdau wa Mbagala akiwa katika harakati za kutafuta chupa kwa ajili ya biashara. Watu mbalimbali wamejiajili wenyewe kwa kufanya biashara za kuuza chupa tupu.
Mfanyakazi wa usafi akitimiza wajibu wake katika harakati za kuliweka jiji safi katika eneo la Mbagala rangi tatu jijini Dar es Salaam leo.
Mama lishe akipika chapati kwa ajili ya wateja wake jirani na rundo la taka katika eneo la Mbagala rangi tatu wilayani Temeke jijijni Dar es Salaam leo.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
FRIDAY, AUGUST 05, 2016 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG ~ MTUMIE RAFIKI YAKO , MAONI: 1
FRIDAY, AUGUST 05, 2016
LUKUVI ATAKA USHIRIKIANO KATIKA UTATUZI WA MIGOGORO YA ARDHI
Mashirika ya kiraia na serikali kwa pamoja yametakiwa kushirikiana na kuratibu shughuli zake kwa ukaribu kushughulikia matatizo na migogoro ya ardhi kwa ufanisi mkubwa.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mjini Morogoro, katika mkutano wa siku mbili uliozikutanisha Tume ya Taifa ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi, iliyo chini ya wizara ya Ardhi na asasi mbalimbali ambazo zenye kujishughulisha na masuala ya ardhi.
Mkutano huo uliohudhuriwa pia na mkuu wa mkoa wa Morogoro, Steven Kebwe, uliangalia mpango wa taifa wa matumizi ya ardhi na mchango wake katika kupunguza migogoro ya archi nchini Tanzania.
Vilevile mkutano huo ulijadili na kuangalia changamoto zilizopo katika masuala ya ardhi hasa upimaji, mipango ya matumizi ya ardhi, na ushiriki wa wananchi wa vijijini hasa wanawake katika utatuzi wa masuala matatizo ya ardhi.
Waziri Lukuvi, alisisitiza kuwepo kwa uratibu wa pamoja shughuli za wadau wa ardhi ili kuwa na dira itakayowezesha utatuzi wa haraka wa matatizo ya ardhi.
Waziri Lukivi amesema jambo hilo litawesesha wadau wa ardhi kufanya uamuzi wa tija katika maamuzi ya sehemu za kwenda zenye migogoro ardhi na kuwafikia wananchi wote.
Mkutano huo uliokutanisha watendaji wa serekali na mashirika ya kiraia, uliandaliwa na Tume ya Taifa ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi, CARE International Tanzania, OXFARM, na Tanzania Resources Forum.
Meza kuu kutoka kushoto Mkurugenzi wa programu ya Maliasiai wa Care International Tanzania Thabit Masoud, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi Dr Steven Nindi, mkuu wa mkoa wa Morogoro Steven Kebwe, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, na Kamishna wa ardhi Bi Mary Makonda.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi Dr Steven Nindi akitoa mada kwa washiriki wa mkutano huo.
Mratibu wa mradi wa Ardhi Yetu wa shirika la CARE International Tanzania, Bi Mary Ndaro, akitoa mada katika mkutano.
Mkurugenzi wa programu ya Maliasili wa Care International Tanzania, Thabit Masoud akitoa mada kwa washiriki.
FRIDAY, AUGUST 05, 2016 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG ~ MTUMIE RAFIKI YAKO , MAONI: 0
FRIDAY, AUGUST 05, 2016
RWANDAIR KUSHUSHA NDEGE MPYA MBILI NA KUONGEZA WIGO WA SAFARI ZAKE
Shirika la ndege la RwandAir linategemea kupokea ndege mpya mbili aina ya Airbus zenye uwezo wa kubeba abiria 274 ifikapo mwezi Septemba 2016, ikiwa na Business class viti 30, Premium Economy Class viti 20 na Economy viti 224. Meneja mkazi wa Shirika hilo hapa nchini, Ibrahim Bukenya amesema ujio wa ndege hizo utaanzisha safari mpya za Bombay nchini India na Guangzhou nchini China. Aliendelea kusema kuwa Shirika hilo litaanzisha safari zake zingine kuelekea Abidjan, Harare, Durban, Abuja, Cotonou na Khartoum.
Meneja mkazi wa Shirika la ndege la RwandAir, Ibrahim Bukenya.
FRIDAY, AUGUST 05, 2016 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG ~ MTUMIE RAFIKI YAKO , MAONI: 0
FRIDAY, AUGUST 05, 2016
KUMBUKUMBU
Leo tarehe 5/8/2016 ni mwaka ,mmoja tangu ututoke ghafla mpendwa Baba, Kaka, Babu, Mjomba Rogers Thomas Maeda. Tunakumbuka upendo wako, hekima, busara na ushauri wako kwetu. Unakumbukwa daima na mkeo Miriam, Baba yako Thomas Maeda, Wanao: Ruth, Rehema, Cathy, Leah, Thomas, Clinton na little Rogers, Kaka yako Humphrey Maeda, Dada zako: Flora, Loveness, Faustina, Haika na Martha, Wapwa zako: Hosea, Thomas T, Lilian, Neema, Emma, Germanus, Gadios, Ruth, Koku, Tumaini, Neema, Mwajabu, Thomas M, Victoria, Veronica, Irene, Godbless, Suzan, Whynjones pamoja na mjukuu wako Brian. Wote tunakukumbuka na tuna imani umepumzika mahali pema peponi pamoja na Mama Ruth, Dada Ida na Dada Mage. Tulikupenda sana lakini Mungu kakupenda zaidi, BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA – JINA LA BWANA LIBARIKIWE.
*Raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umuangazie – upumzike kwa Amani*.
AMEN.
FRIDAY, AUGUST 05, 2016 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG ~ MTUMIE RAFIKI YAKO , MAONI: 0
FRIDAY, AUGUST 05, 2016
INTRODUCING MUVIKA ONLINE: KUTAZAMA AU KUPAKUA FILAMU UZIPENDAZO
FRIDAY, AUGUST 05, 2016
WANANCHI MKURANGA WASHAULIWA KUCHUKUA SHAMBA LENYE UKUBWA WA HEKARI 66.6 AMBALO ALIPEWA MWEKEZAJI TANGU MWAKA 1988
Wananchi wa kijiji cha Kurutu kilichopo kata ya Shungubweni wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani wameshauliwa kuchukua shamba lenye ukubwa wa hekari 66.6 ambalo alipewa mwekezaji tangu mwaka 1988 na kushindwa kuliendeleza,ili walitumie Kwa shughuli za kuzalisha mali.
Ushauri huo ulitolewa wilayani humo na Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Abdallah Ulega mara baada ya kupokea malalamiko kutoka Kwa wananchi wake akiwa katika ziara zake za kushukuru wanakijiji hao Kwa kumchagua kuwa mbunge wao.
Ulega alisema haiwezikani watu wanajimilikisha mashamba makubwa miaka hadi miaka alafu wanashindwa kuyaendeleza huku wananchi wakipata shida ya kukosa maeneo hata ya kulima kilimo cha mbogamboga vijana.
"Nasema kuwa kama shamba hilo limekaa miaka yote hiyo haliendelezwi, na pia huyo mwekezaji haonekani sasa mnasubiri nini kulichukua na kufanya uendelezaji. Nashauri litwaeni halafu tutapambana naye huko mbele"
Pia Ulega aliwaeleza wananchi hao kuwa siasa imekwisha na kilichobaki ni watu kufanya Kazi Kwa nguvu zote na kwamba atakuwa bega Kwa bega katika kuhakikisha maendeleo wanayapata Kwa haraka.
Awali wananchi wa kijiji cha Kurutu walimweleza mbunge kuwa wanavshamba kubwa ambalo alipewa mwekezaji miaka mingi iliyopita tena kienyeji lakini hadi leo ameshindwa kuliendeleza hivyo awasaidie walipate ili vijana wa eneo hilo wazalishe chumvi.
Mbunge huyo bado anaendelea na ziara zake za kutembelea kijiji hadi kijiji kwa lengo la kuwashukuru na kuhimiza shughuli za maendeleo ambapo anawataka kujituma katika kufanya kazi kwani wilaya hiyo imechelewa kimaendeleo.
Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mhe Abdallah Ulega akielekea kijiji cha Kurutu kilichopo kata ya Shungubweni wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani kwa mtumbwi.
Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega akikagua daraja
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na walimu wa shule ya msingi ya kijiji cha Kurutu kilichopo kata ya Shungubweni
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kurutu kilichopo kata shungubweni wilayani Mkuranga katika ziara zake za kushukuru wanakijiji hao Kwa kumchagua kuwa mbunge wao.
Mwanakijiji Shabani Omary akiuliza swali kwa mbunge wa jimbo la mkuranga Mhe. Abdallah Ulega. Habari na picha na Emmanuel Masaka wa Globu ya Jamii
FRIDAY, AUGUST 05, 2016 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG ~ MTUMIE RAFIKI YAKO , MAONI: 1
FRIDAY, AUGUST 05, 2016
SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI
SIMU.TV: Serikali imeazimia kuvilinda viwanda vya ndani ili viweze kuzalisha bidhaa zinazoweza kushindana na bidhaa zinazotoka nje ya nchi. https://youtu.be/4t4ry8opqzk
SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametoa kiasi cha laki moja na nusu kwa ajili ya matibabu ya mkazi wa Temeke jijini Dar es salaam.https://youtu.be/x06ZDLBIHzs
SIMU.TV: Kamati ya usalama barabarani imekuja na utaratibu wa kuweka alama kwenye leseni za madereva watakaosababisha ajali barabarani. https://youtu.be/pa7yiwAH2Tc
SIMU.TV: Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee, watoto na walemavu Ummy Mwalimu, ameitaka mamlaka ya uthibiti wa dawa na chakula kuthibiti dawa zote feki zinazoingia nchini. https://youtu.be/0550oV3Shq4
SIMU.TV: Maonesho ya nane nane yameendelea kuwa chachu ya wananchi kuelimika na kupata fursa ya kujua miradi ya maendeleo inayofanywa na serikali.https://youtu.be/0Cp12JKWpQ8
SIMU.TV: Serikali imeagiza kufanyika kwa uchunguzi wa kina ili kubaini gharama halisi zilizotumika kujenga jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe.https://youtu.be/WIxASSdZQu4
SIMU.TV: Serikali imesema itaendelea kuzisaidia na kuziunga mkono taasisi za fedha zilizojikita katika kuinua wananchi wahali ya nchini kiuchumi.https://youtu.be/ZOMbWGMwS2w
SIMU.TV: Naibu waziri ofisi ya rais TAMISEMI amewataka wananchi wanaosubiri ajira mpya na watumishi wanaosubiri kupandishwa vyeo kuwa na subira, maana serikali inakaribia kumaliza zoezi la uhakiki wa watumishi. https://youtu.be/HiVR2K-UN70
SIMU.TV: Wananchi katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wamelalamikia wafugaji kuvamia mashamba yao na kuwatishia maisha yao. https://youtu.be/p6y-GwJ1OVA
SIMU.TV: Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini TAKUKURU imethibitisha kumkamata rais wa klabu ya Simba Evance Aveva kwa tuhuma za rushwa.https://youtu.be/2M5dGtrNXYg
SIMU.TV: Mabingwa wa soka Tanzania bara timu ya Yanga pamoja na timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu zimekabidhiwa vifaa vya michezo na wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom. https://youtu.be/KcdOcLkCUzw
SIMU.TV: Timu ya Serngeti boys imewasili nchini Afrika Kusini ikitokea nchini Madagascar ilikokuwa imeweka kambi kwa ajili ya mchezo wake na timu ya vijana ya Afrika Kusini.https://youtu.be/h5v0O_OKgt4
FRIDAY, AUGUST 05, 2016 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG ~ MTUMIE RAFIKI YAKO , MAONI: 0






No comments:
Post a Comment