Gadget
| This content isn't available over encrypted connections yet. |
SATURDAY, AUGUST 20, 2016
JK AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KWENYE MAZISHI YA BI SHAKILA MBAGALA CHARAMBE JIJINI DAR.
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Bi Shakila Said,wakati wa maziko huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2016.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye akiweka udongo kwenye kaburi la Bi Shakila Said,wakati wa maziko huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar.
Rais Mstaafu awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo cha Bi Shakila Said ,huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar,wa pili kushoto aakishuhudia ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye na Katibu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw. John Kitime.
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiweka saini kitabu cha maombolezo cha Bi Shakila Mbagala Charambe,jijini Dar es salaam. Kushoto ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye.
Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo cha Bi Shakila Said huko nyumbani kwa marehemu Mbagala Charambe,jijini Dar es salaam.
Rais Mstaafu awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete (wa pili kulia) na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye (pili kushoto) wakishiriki maziko ya aliyekuwa Mkongwe,mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarabu hapa nchini,Bi Shakila Saidi ambaye mazishi yake yamefanyika leo huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar.
SATURDAY, AUGUST 20, 2016
JESHI LA POLISI LAPIGA MATIZI YA UTAYARI WA KUKABILIANA NA MATUKIO YA UHALIFU NA WAHALIFU NCHINI
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wa wakiwa moja ya maozezi yao ya kupasha viungo kabla ya kuanza mazoezi ya kutuliza ghasia.
Askari Polisi wa kikosi maalum cha polisi (CRT) wa mkoa wa Iringa wakiwa katika mazoezi ya utayari wa kukabiliana na matukio yoyote yatakayojitokeza katika maeneo mbalimbali.
Askari wa vikosi vya kutuliza ghasia wa mikoa mbalimbali wakiwa na magari yao wakati wa mazoezi ya utayari wa kupambana na matukio mbalimbali ya uhalifu na wahalifu katika maeneo mbalimbali.
Askari wa vikosi vya kutuliza ghasia wa wakiwa na magari yao wakati wa mazoezi ya utayari wa kutuliza ghasia na kukabiliana na matukio yoyote ya uhalifu na wahalifu.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
SATURDAY, AUGUST 20, 2016
KAMANDA MPINGA MGENI RASMI SHINDANO LA USALAMA BARABARANI KWA SHULE ZA MSINGI
SATURDAY, AUGUST 20, 2016
PICHA ZA MWISHO ZA MWASISI WA TAARABU MAREHEMU SHAKILA SAID MJINI DODOMA
Aliyekuwa msanii mahiri wa Taarab, marehemu Shakila Said wakati wa uhai wake akipongezwa na Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa Tamasha la wasanii la kumuaga Mhr. Kikwete baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa chama hicho, mjini Dodoma Julai 23, mwaka huu.
Shakila akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Abdulrahman Kinana
Aliyekuwa msanii mahiri wa Taarab, marehemu Shakila Said wakati wa uhai wake akiwa kwenye hafla hiyo
(PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
SATURDAY, AUGUST 20, 2016 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG ~ MTUMIE RAFIKI YAKO , MAONI: 1
SATURDAY, AUGUST 20, 2016
MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA WATENDAJI WA IDARA YA MAZINGIRA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mkutano wa kazi na watendaji wa ofisi yake ya Idara ya Mazingira kujadili kwa kina namna ya kukabiliana na hali tete ya uharibifu wa mazingira unaoendelea nchini.
Katika mkutano huo uliofanyika leo, Ikulu, Dar es salaam ambao ulihudhuriwa pia na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba, Makamu wa Rais ameawaagiza watendaji wa idara hiyo waache kukaa ofisini na badala yake waende kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini.
Alisema hali ya uharibifu wa mazingira ikiachwa iendelee kama ilivyo inaweza ikasababisha madhara makubwa kwa jamii na Taifa kwa ujumla, hivyo ni muhimu kwa makundi yote wakiwamo wataalam wa mazingira na wadau wa maendeleo kuelekeza nguvu zao katika kukabiliana na tatizo hilo.
Alisema baadhi ya watendaji wamekuwa ni sehemu ya uharibifu wa mazingira na kuonya wataobainika kufanya vitendo hivyo watachukuliwa hatua kali ili kukomesha tabia hiyo.Baadhi ya watendaji waliotoa taarifa kuhusu hali ya mazingira nchini wamekiri kuwa hali ya uharibifu wa mazingira siyo nzuri hasa kwenye mikoa ya Dodoma, Shinyanga, Manyara, Geita, Singida na Kilimanjaro.
Inakadiriwa kuwa takribani hekta 400,000 za misitu zinaharibiwa kila mwaka hali ambayo inapelekea baadhi ya wanyama kutoweka.Watendaji hao wameiomba serikali iongeze bajeti ya kutosha ili waweze kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira ikiwemo utoaji wa elimu kwa wananchi.Makamu wa Rais ametumia siku ya mapumziko ili kujadiliana na kuweka mipango na mikakati ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira nchini. Mkutano huo wa kazi unaendelea tena hapo kesho.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa mkutano na Watendaji wa Ofisi yake Idara ya Mazingira mara baada ya kupata taarifa za maendeleo, mipango na mikakati ya Idara hiyo, kulia ni Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifafanua jambo kwenye mkutano wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Watendaji wa Idara ya Mazingira (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa mkutano na Watendaji wa Ofisi yake Idara ya Mazingira Ikulu jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa mkutano na Watendaji wa Ofisi yake Idara ya Mazingira, kushoto ni Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na kulia ni Katibu Mkuu Oisi ya Makamu wa Rais Bw. Mbaraka Abduwakil Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Msaidizi Idra ya Mazingira Bi. Esther Makwaia akiwasilisha taarifa ya hali ya Mazingira nchini kwenye mkutano na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu, Ikulu jijini Dar es Salaam.
SATURDAY, AUGUST 20, 2016
WAZIRI MKUU MAJALIWA AWASILI MPANDA KWA ZIARA YA KIKAZI MKOANI HUMO EO
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Mkoa wa Katavi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda kuanza ziara ya kikazi mkoani humo leo Agosti 20, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Vijana wa CCM baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda kuanza ziara ya kazi mkoani Katavi leo Agosti 20, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wananchi wa mkoa wa Katavi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda kuanza ziara ya kazi mkoani humo leo Agosti 20, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wananchi wa mkoa wa Katavi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda kuanza ziara ya kazi mkoani humo leo Agosti 20, 2016.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
SATURDAY, AUGUST 20, 2016 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG ~ MTUMIE RAFIKI YAKO , MAONI: 0
SATURDAY, AUGUST 20, 2016
SIMBA AUNGURUMA TAIFA LEO, WAITANDIKA NDANDA FC BAO 3-1
Mshambuliaji wa Timu ya Simba, Shiza Kichuya akiachia shuti lililopelekea kuipatia Timu yake bao la tatu dhidi ya Timu ya Ndanda, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Simba imeshinda Bao 3-1.

Mshambuliaji wa Timu ya Simba, Shiza Kichuya akishangilia Ushindi sambamba na Mashabiki wa Simba baada ya kuipatia timu yake bao la tatu dhidi ya Timu ya Ndanda, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Simba imeshinda Bao 3-1.
Mshambiaji wa Simba, Laudit Mavugo akiondoka na kijiji cha wachezaji wa Ndanda katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Simba imeshinda Bao 3-1.
Kipa wa Simba, Vincent Agban akiruka na kuusindikiza kwa macho mpira ukiingia wavuni baada ya kupigwa kichwa safi kabisa na Mshambuliaji wa Timu ya Ndanda, Omary Mponda na ikiwa ni goli la kufutia machozi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Simba imeshinda Bao 3-1.
Beki wa Simba, Mohamed Hussein akiondoka na mpira.

No comments:
Post a Comment