Wednesday, 3 August 2016

There was an error in this gadget

EAST AFRICA VIBES CONCERT THIS SATURDAY AT NAFASI! TICKETS ON SALE NOW!

Mambo Art Lovers,
Mambo vipi wapenzi wa sanaa,
Hope your July was exciting as ours!
Ni matumaini yetu umekuwa na mwezi Julai wa kustaajabisha!
We’re very excited about the East Africa Vibes Concert happening this Saturday right here at Nafasi Art Space. Tickets are on sale now -- you can get yours at Nafasi today or book online at: www.timetickets.net
Tuna shahuku kubwa kuhusiana na Tamasha la East Africa Vibes litakalofanyika Jumamosi hii hapa Nafasi Art Space. Sasa Tiketi zinauzwa - Unaweza kununua hapa Nafasi leo au weka oda kupitia mtandaoni: www.timetickets.net
The concert will feature live performances by Oliver “Tuku” Mtukudzi (Zimbabwe), Eric Wainaina (Kenya), Slim Emcee (Uganda), Wahapahapa Band (Tanzania) and many more. Tickets are just 50,000tsh VIP and 20,000tsh general admission.
We hope to see you on Saturday!
Tamasha litahusisha Musiki wa moja kwa moja kutoka kwa "Tuku" Mtukudzi (Zimbabwe), Eric Wainaina (Kenya), Slim Emcee (Uganda), Wahapahapa Band (Tanzania) na wengine wengi. Tiketi Maalumu ni Sh 50,000/ tu! na Za kawaida ni
Sh 20,000/. Tuna tegemea kukuona Siku hiyo ya Jumamosi!


WAZIRI MAHIGA ATEMBELEWA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UFARANSA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akimpokea rasmi Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mhe. Jean-Marc Ayrault (kushoto) alipotembelea Wizarani katika ziara yake ya kikazi nchini. Mazungumzo kati yao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ufaransa ili kuchangia maendeleo ya nchi hizi mbili. Pia Waziri Mahiga alitumia fursa hiyo kumpa salamu za pole kutokana na mashambulio ya kigaidi yaliyotokea nchini Ufaransa hivi karibuni. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2016. 
Wajumbe waliofuatana na Mhe. Waziri Aryault nao wakifuatilia mazungumzo. Kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Malika Berak.
Mazungumzo yakiendelea.

WATUMIAJI WA MABASI YA MWENDO KASI WARAHISISHIWA ULIPIAJI WA KADI ZAO.

·         Ni kupitia huduma ya Vodacom M-PESA kwa kushirikiana na Maxcom Africa.
Jumatano, AGOSTI 3 2016, Watumiaji wa mabasi ya mwendo kasi warahisishiwa jinsi ya kulipia kadi zao za kusafiria,Haya yametokana na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kwa kuingia ubia na kampuni ya Maxcom Africa kwa kuhakikisha kutoa huduma zilizobora kwa watumiaji wote wanaotumia usafiri huo  kwa kuweza kuongeza Salio kwenye kadi zao za kusafiria za DART kwa urahisi zaidi kupitia huduma ya M PESA.

 Huduma hii imeanza rasmi tarehe 1 Agosti 2016 inayowalenga watumiaji wote wa mabasi ya mwendo kasi jijini Dar es salaam.

Akiongelea huduma hii Sitoyo Lopokoiyit, Afisa mtendaji mkuu wa huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania, alisema ‘M-Pesa imeongeza wigo zaidi na unafuu kwa watumiaji wa mabasi haya mbali na njia nyingine zilizokuwa zikutumika kama Mawakala wa Maxmalipo au kwenye vituo mbalimbali vya mabasi ya Mwendo kasi (DART). Ushirikiano kati ya Vodaco,  Maxcom na DART ni muendelezo wa juhudi za kuhakikisha kwamba huduma ya M-Pesa inaendelea kumrahisishia na kumboreshea  maisha ya kila siku mtanzania’

Naye Mkurugenzi wa Maxcom Africa ,Juma Rajabu alisema ‘Mfumo uliowekwa na Max malipo kwenye usafiri huu wa Mabasi ya mwendo kasi ni Mfumo wa kisasa  na salama zaidi unaotumia Kadi maalumu pamoja na Tiketi zenye QR codes, pia Mfumo huu umeboreshwa zaidi kwa kuunganishwa na Makampuni za mawasiliano kama Vodacom Tanzania ambapo wasafiri bila kupoteza muda wanaweza kuweka Salio katika kadi zao za kusafiria kupitia huduma iliyo bora nay a uhakika ya M PESA. Kwa mara ya kwanza duniani na Africa kwa ujumla,Vodacom Tanzania inaingia kwenye kitabu cha historia kwa kuwa kampuni ya kizalendo iliyoleta mapinduzi katika Sekta ya Usafiri’

David Mgwassa, Mkurungezi mkuu wa UDART alisema Matumizi ya kadi ni muendelezo wa utambuzi wa Tanzania, kwenye kuelekea maisha ya kisasa. ‘Kadi ya DART inamsaidia abiria kuondoa kero ya kutembea na pesa taslimu na kupanga foleni kwani inamuwezesha kulipia nauli kabla ya safari. 

Uwezo wa kutumia simu yake ya mkononi unaondoa  usumbufu wa kupanga foleni kwenye vituo vya mabasi ya mwendo haraka. Kizuri zaidi ni kwamba kadi hii inaweza kujazwa kiwango chochote cha fedha kisichozidi shilingi 30,000 kwa wakati mmoja na haina muda wa kikomo wa matumizi na fedha inayokuwa ndani ya kadi itaendelea kuwemo kwenye kadi bila kikomo mpaka mhusika atakapoitumia’
Kuongeza salio kwenye kadi yako DART kupitia M-Pesa fuata hatua rahisi zifuatazo;
1.       Piga *150*00# chagua LIPA KWA M-PESA,
2.       Chagua DART,
3.       Weka namba ya kumbukumbu ambayo ni namba ya kadi yako ya DART
4.       Weka KIASI (Mfano 2000, 5000, 10000 n.k),
5.       Weka PIN yako ya M-Pesa
6.       Bonyeza 1 kukamilisha muamala. Utapokea ujumbe mfupi kuthibitsha muamala wako.

Aidha, katika hatua nyingine, UDART wameshusha bei ya kadi kutoka shilingi 5,000 ya awali mpaka shilingi 2,000 kwa maana ya bei ya kadi shilingi 500 na nauli ya kuanzia shilingi 1,500.

KITUO CHA WATOTO WACHANGA YATIMA NJOMBE CHAOMBA MSAADA WA MASHINE YA KUFULIA.

Baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha kulelea watoto wachanga Yatima na lishe cha kipengere Mkoani Njombe wakifua nguo za watoto kwa mikono baada ya mashine walizokuwa wakizitumia kuharibika, Picha na James Festo.

Na James Festo, Njombe. 

KITUO cha kulelea watoto yatima na lishe cha Kipengere kinachopatikana wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe ambacho huwahumia watoto wachanga yatima wenye umri wa miaka 0 hadi mitano kimewaomba wadau kusaidia kununua na kutengeneza mashine ya kufulia kutokana na zilizokuwapo kuharibika baada ya kutumika muda mrefu. 

Msimamizi wa kituo hicho ambacho kwa sasa kinawahudumia watoto 51 miongoni mwa 220 ambao waliwahi kuhudumiwa na kituo hicho, Sister Nivardina Mbifile aliliambia gazeti hili mwishoni mwa juma kwamba kwa sasa hulazimika kuamka saa kumi na moja asubuhi kufua nguo za watoto tofauti na hapo kabla. 

""tunachangamoto kubwa sana ya mashine ya kufulia, tulikuwa nazo zimezeeka zimeharibika sasa tunafua nguo kwa mikono sasa watoto ni wengi tunaamka saa 10 kufua nguo za watoto hadi jioni tulionao ni wachanga ...hapo mwanzo tulikuwa na mashine hata wafuaji walikuwa wanapata nafuu...sasa hivi mikono inachubuka kwa sasa" alisema Sister Mbifile. 

Aliongeza kuwa "mashine hizi mbili zilishawahi kusumbua na tulisubiri wataalamu kutoka nje ya nchi wakaja kututengenezea zikaendelea kufanya kazi na sasa hatuwezi kutengeneza tena...na hii moja haina mda mrefu tumeacha kuitumia kwa sababu ilianza kuleta maneno ya kichina hivyo tunasubiri wataalamu kutoka nje wakiwahi watakuwa wametusaidia sana ila tunaomba mwenye uwezo wa kutusaidia atusaidie. 

Umoja wa wananchi wa Njombe Magharibi waishio jijini Dar es salaam UWENDE ni miongoni mwa waliofika kutoa msaada ya vyakula na mahitaji muhimu kwa watoto yatima katika kituo hicho wakiongozwa na Pascal Ngilangwa wenye thamani ya shilingi milioni 1.08 wakizungumza baada ya kuzungumza na wafuaji wa Nguo za watoto ambao wengi ni wachanga walisema msaada wa mapema unahitajika. 

"kufua kwa mkono nguo za watoto ambao baada ya saa moja huwa hazitazamiki kama nepi ni jambo linalohitaji moyo tena si kidogo tunaomba wadau wengine wasaidie kupatikana kwa mashine ya kufulia... hata viongozi wa serikali wasaidie hadi Rais wangu Magufuli mimi namlilia aje asaidie kutengeneza mashine au kununua mashine ya kufulia" alisema Ngilangwa. 

Aliongeza kuwa "sisi tumeamua kujitolea msaada ni jadi yetu tumekuwa tukisaidia kwenye upande wa elimu, kilimo, afya na mazingira sisi huchangishana na kutoa misaada hii kila mwaka katika maeneo mbalimbali. 

Kulingana na Sister Mbifile sehemu kubwa ya watoto ambao hulelewa kituoni hapo wamewapoteza wazazi wao kutokana na ugonjwa wa ukimwi pamoja na matatizo ya uzazi wakati wanapojifungua na asilimia kubwa ni kutoka wilaya za Makete, Njombe na Wanging'ombe. Itakumbukwa Mkoa wa Njombe kwa sasa ndio unaongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi kinachofikia asilimia 14.8 kulingana na utafiti wa Tume ya kudhibiti ugonjwa wa Ukimwi humu Nchini TACAIDS iliyotolewa mwanzoni mwa muongo wa pili wa karne ya 21

No comments:

Post a Comment