Thursday, 18 August 2016

JWTZ WATWAA MAKOMBE RWANDA

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

KAMATI ZA BUNGE KUANZA VIKAO VYAKE AGOSTI 22, 2016


WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA BALOZI WA ISRAEL NCHINI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Israel Nchini Tanzania Mh. Yahel Vilan alimpomtembelea Ofisini kwake barabara ya Luthuli jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akijadiliana jambo na Balozi wa Israel Nchini Tanzania Mh Yahel Vilan alimpomtembelea Ofisini kwake barabara ya Luthuli jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni Maafisa toka Wizara ya mambo ya nje waliongozana na Balozi huyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akisoma Nakala za machapisho alizopatiwa na Balozi wa Israel Nchini Tanzania Mh . Yahel Vilan.

VIJANA ELFU 18 KUSOMA UFUNDI STADI KWA SIMU KUPITIA AIRTEL FURSA VSOMO

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na VETA imeingia mkoani Arusha kuendelea kutoa uelewa kwa vijana kukamata FURSA na kusomo kozi mbalimbali toka VETA kupitia mfumo wao wa simu ujulikanao kama VSOMO. hadi sasa zaidi ya vijana elfu kumi na nane nchini wamejisajili kusoma kwa mfumo huo wa simu za mkononi huku mikakati yao ikiwa ni kuongeza kozi 10 zaidi ili wanafunzi kuendelea kujisomea.

Hayo yamebainishwa na  Mkuu wa mauzo kanda ya kaskazini  Bw, Brighton Majwala wakati alipoongea na wajasiliamali na madereva bodaboda  waliokusanyika stand kuu  Arusha jana,   

“Airtel na Mamlaka ya ufundi stadi VETA lengo letu ni kuwafikishia elimu ya ufundi vijana wengi nchini, upande wetu Airtel tunahakiksha mtandao upo vyema ili vijana waweze kusoma bila kukwama, hadi leo hii tayari vijana zaidi ya milioni 18 wameshakamata FURSA hii kwa kupakua aplikesheni au mfumo huu wa VSOMO katika simu zao” alieleza Bw Majwala

Majwala aliendelea kusema kuwa “mpango wetu Airtel na VETA ni  kuongeza uelewa kwa  vijana ili wasome kozi zilizopo sasa ikiwemo ya  ufundi piki piki, umeme wa nyumbani, ufundu simu, ufundi wa aluminium, utaalam wa masuala ya urembo, pamoja na ufundi wa kuchomea vyuma”.

kwa upande wake Meneja  Uhusiano wa Airtel alisema “kutokana na VSOMO kuwa na idadi kubwa ya vijana waliojisajili  tayari Airtel kwa kushirikiana na wadau wetu VETA tuko katika utekelezaji wa kuongeza kozi zingine zaidi ya kumi ili kuongeza wigo wa kuchagua pamoja na kuongeza  idadi ya wanaosoma na kuhitimu”. alieleza mmbando

“tunampango wa kuongeza kozi zingine 10 kabla ya mwezi wa 12 ambapo sasa hivi tayari VETA wako katika utaratibu wa kuzifanyia kazi kozi hizo ili ziweze kuingia katika mtandao” alisema Mmbando

 “Mradi wa VSOMO ni sehemu ya mpango wa Airtel FURSA wenye lengo la kuwawezesha vijana pamoja na kutimiza kauli mbiu ya  “Airtel the smartphone network” kwa kujipatia elimu ya ufundi stadi toka VETA kwa smartphone zao” alisisitiza Mmbando

Airtel kwa kushirikiana na  VETA nchini ilizindua mfumo wa masomo ya ufundi stadi kwa njia ya mtandao VSOMO mwezi Julai 2016 ambapo mpaka sasa  tayari mfumo huu umetambulishwa  katika mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Arusha, Morogoro na Mwanza lakini kutokana na uhitaji mkubwa kwa  vijana tayari mfumo huo umepokea maombi ya vijana toka mikoa 25  kwa kupakua mfumo/aplikesheni hiyo hiyo na kuomba kusoma kwa njia ya simu za Airtel.
Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando (katikati) akitoa maelekezo kwa baadhi ya wanaotoa huduma ya usafiri wa Boda boda Arusha eneo la stand kuu Arusha jinsi wanavyoweza kujiunga na mfumo wa VSOMO na kusoma masomo ya Ufundi stadi kupitia mtandao wa Airte jana.
Mkuu wa mauzo wa Airtel kanda ya kaskazini Bw, Bryton Majwala na wafanyakazi wengine wa Airtel kwa pamoja wakizungumza na baadhi ya wajasiliamali na watoa huduma ya usafiri wa Boda boda Arusha eneo la stand kuu Arusha jinsi wanavyoweza kujiunga na mfumo wa VSOMO na kusoma masomo ya Ufundi stadi kupitia mtandao wa Airtel jana.
Mkuu wa mauzo wa Airtel kanda ya kaskazini Bw, Bryton Majwala akitoa maelekezo kwa baadhi ya wajasiliamali wanaotoa huduma ya usafiri wa Boda boda Arusha eneo la stand kuu Arusha jinsi wanavyoweza kujiunga na mfumo wa VSOMO na kusoma masomo ya Ufundi stadi kupitia mtandao wa Airtel mkoani jana.

MGODI WA DHAHABU WA BULYANHULU WATENGENEZA AJIRA KWA WAJASILIAMALI VIJIJINI KUPITIA MRADI WA MADAWATI

Afisa Mahusiano wa Mgodi wa Bulayanhulu Sara Teri (kulia)  na Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Bulayanhulu Elias Kasitila wakikabidhi madawati kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Hamim Gwiyama pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya Nyangw’ale.
Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Bulyanhulu uliopo mkoani Geita ,Elias Kasitila akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya madawati yaliyotolewa na mgodi huo kwa ajili ya shule zilizoko katika wilaya ya Nyang'wale.
Utengenezaji wa Madawati ulitoa fursa ya ajira kwa fundi Deus Mlela aliyepewa tenda na Mgodi wa Bulyahulu ya kutengeneza madawati mia tano.


DC KASESELA AKUTANA NA MASELA WA KIHESA, MJINI IRINGA, APIGA JALAMBA NA MGAMBO

Katika kupunguza kasi ya uhalifu na kuwawezesha Vijana wa Iringa, Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alikutana na vijana wa kijiwe cha Kihesa, ambao wengi wao wanajishughulisha na kuosha magari na kuwaomba kusaidiana naye katika kutokomeza udokozi.

Vijana hao walimuomba Mkuu wa Wilaya awasaidie upatikanaji wa mashine ya kuoshea magari ambayo aliwahidi kuwatafutia ndani ya siku 2 ili mradi wajiunge kwenye kikundi na wafungue akaunti benki. Vijana hao walimsukuru sana mkuu wa wilaya na kuahidi kuwa watiifu wa sheria na kuchapa kazi. Kikundi hicho kina vijana 25.
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akifanya mazungumzo na Kikundi cha vijana 25 wanaojishughulisha na uoshaji wa magari katika eneo la Kihesa, Mjini Iringa.
Kasesela akipitia taarifa ya Kikundi hicho aliyokabidhiwa.
Akitoka eneo hilo baada ya kumaliza kuzungumza na vijana hao.


UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETI YA LEO


IGP MANGU AWAAGA ASKARI 14 WA KIKOSI MAALUM CHA POLISI (S.F.U)

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akimuuaga PC Prosper Yenda yenda wa kikosi maalum cha Jeshi la Polisi ( S.F.U) ambaye ni miongoni mwa askari 14 wanaokwenda nchini Jordan kwa kozi maalum ya kupambana na uhalifu na wahalifu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akiwa katika picha ya pamoja na askari 14 wa kikosi maalum cha Jeshi la Polisi (S.F.U) ambao wanaokwenda nchini Jordan kwa kozi maalum ya kupambana na uhalifu na wahalifu. (Picha na Tamimu Adam- Jeshi la Polisi).

WAZIRI MKUU AWAWEKA SAWA WATUMISHI WA OFISI YAKE, TAYARI KWA SAFARI YA DODOMA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema safari ya kuhamia Dodoma imeiva na amewataka watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wajipange kisaikolojia.

Ametoa kauli hiyo jana (Jumatano, Agosti 18, 2016) alipokutana na kuzungumza na watumishi wa ofisi yake kutoka taasisi, idara na vitengo mbalimbali waliopo Dar es Salaam.

Waziri Mkuu aliwataka watumishi hao watambue kuwa uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao chimbuko lake ni agizo lililotolewa Oktoba Mosi, 1973 kwenye Mkutano Mkuu wa 16 wa chama cha TANU.

“Tangu wakati huo kumekuwa na juhudi mbalimbali zilizofanyika ili kuandaa miundombinu na hata awamu ya nne ilisimamia kwa kiwango kikubwa uwekaji wa miundombinu hiyo,” alisema.

“Pia tukumbuke kauli ya Mheshimiwa Rais aliyotoa kwenye hotuba yake ya Julai 23, 2016 alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM, na akairudia tena Julai 25, kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa na mimi siku hiyo hiyo nikaweka msisitizo,” alisema.

“Napenda kuwatoa hofu, mambo yanaenda vizuri ila mtambue kuwa safari imeiva sasa. Kikubwa ni kwamba tutakwenda kwa awamu kama ambavyo imepangwa,” alisema.

Aliwataka watumishi hao wazidishe mshikamano miongoni mwao huku wakitambua kuwa wana dhamana ya kuwatumikia Watanzania kwa uadilifu na uaminifu. “Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu tunapaswa tutambue dhamana tuliyonayo. Tufanye kazi kwa bidii. Tuhakikishe kila kilichopangwa kinafanyika kwa ufanisi na kinafanikiwa,” alisema.

JWTZ YANYAKUA VIKOMBE VITATU MASHINDANO YA MAJESHI MJINI KIGALI

Mnadhimu mkuu wa Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania Luteni Generali Venance mabeyo akisalimiana na wachezaji wa timu ya Soka ya Tanzania wakati wa mchezo wa mwisho dhidi ya Rwanda Tanzania ilifungwa bao 1-0 na kushika nafasi ya tatu
Mwanariadha Siata Kalinga akipokea kikombe cha mshindi wa tatu kwa riadha wanawake kutoka kwa Naibu Mkuu wa Majeshi wa Uganda Luteni Jenerali Charles Angina.
Viongozi waandamizi wa majeshi waliowakilisha wakati wa sherehe za kufungwa mashindano ya   Majeshi kwa nchi za Afrika Mashariki, yaliyokuwa yakifanyika Mjini Kigali nchini Rwanda kutoka kulia ni mkuu wa majeshi wa Rwanda Jenerali Patrick Nyamvumba, akifuatiwa na Mkuu wa majeshi wa Kenya Jenerali Samson Mwathethe, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Venance Mabeyo pamoja na Naibu Mkuu wa Majeshi wa Uganda Luteni Jenerali Charles Angina. (picha na Selemani Semunyu)

No comments:

Post a Comment