Tuesday, 30 August 2016

ARUDI SHULE

MTOTO ALIYENENEPA ZAIDI DUNIANI ARUDI SHULENI BAADA YA KUPUNGUZA UZITO

Mtoto wa miaka 10 kutoka Indonesia, ambaye ametajwa kuwa mtoto aliyenenepa zaidi duniani alianza kupewa chakula cha kupunguza uzito Arya Permana ameorodheshwa kuwa na unene usio wa kawaida kwa kuwa alikuwa na uzani wa kilo 188.

Mtoto huyu hatimaye ameweza kurudi shuleni baada ya kupunguza uzito wa kutosha wa kumwezesha yeye kutembea kwani siku zote alikuwa akillala na hakuweza kutembea na kusababisha yeye kukatisha masomo.

Mtoto huyu unaambiwa amekuwa akila milo mitano kwa siku lakini baada ya ushauri wa kufanya diet na mazoezi makali Arya ameanza kupunguza uzito ndani ya wiki chache sasa anaweza kukaa lakini pia kutembea kwenda shule na kucheza na wenzake darasani










LOWASSAAAAAA

Lowassa, Mbowe Watakiwa Kuripoti Polisi Leo

Viongozi waandamizi wa Chadema akiwamo Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana walikamatwa na Jeshi la Polisi wakati wakiwa katika kikao cha ndani katika Hoteli ya Giraffe mkoani Dar es Salam.

Lowassa, ambaye alikaa kituoni hapo kwa takribani saa tatu anaweza kuwa kiongozi wa kwanza aliyewahi kushika nafasi ya Waziri Mkuu kuhojiwa na polisi.

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu aliwataja viongozi wengine waliokamatwa kuwa ni Mwenyekiti, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Issa.

Mara baada ya kukamatwa, walipelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi ambako baadhi ya wajumbe na wabunge waliwafuata na kuwasubiri nje ya kituo hicho kujua hatima yao.

Viongozi hao walionekana wakiingia Polisi saa 10.30 jioni na kutoka saa 1.25 usiku, jambo ambalo liliwafanya wakae kituoni hapo kwa saa tatu.

Lissu alisema polisi walivamia kikao hicho kilichokuwa na wajumbe 170, wakiwamo baadhi ya wabunge wa chama hicho na kuwakamata viongozi hao kwa maelezo kuwa wamekaidi amri ya Jeshi la Polisi ya kuzuia mikutano ya ndani na nje ya vyama vya siasa.

Imeelezwa kuwa viongozi hao wa Chadema walikuwa na mkutano uliotanguliwa na kikao cha viongozi wakuu na kufuatiwa na cha viongozi hao kikijumuisha wabunge, mameya na wenyeviti wa halmashauri.

Wakiwa katika kikao hicho, ilielezwa kuwa watu wanne waliingia wakiwa wamevalia kiraia na kuwaeleza kuwa viongozi wao wanahitajika kituo kikuu cha polisi kutokana na kufanya mkutano kinyume cha sheria.

Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo Peneza ambaye  alikuwa kwenye mkutano huo alisema pamoja na mambo mengine ya chama, walikuwa wakijadili suala la operesheni Ukuta la Septemba Mosi kama liendelee au lisiendelee kutokana na hali ilivyo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alipoulizwa kuhusu kukamatwa kwao, alisema viongozi hao walikamatwa kwa kukukaidi amri ya polisi ya kuzuia mikusanyiko ya kisiasa na kuchochea wananchi kuandamana kinyume cha sheria Septemba Mosi.

Alisema baada ya kuachiwa kwa dhamana, viongozi hao wametakiwa kuripoti kituoni hapo leo.

Wiki iliyopita, Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamishana wa Operesheni na Mafunzo, Nsato Marijani lilipiga marufuku mikutano ya ndani likisema inatumika kuhamasisha watu kuvunja sheria za nchi na kupambana na askari.

Hatua hiyo ilikuja huku jeshi hilo likiwa limepiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano kufuatia uamuzi wa Rais John Magufuli kuzuia shughuli  za kisiasa hadi 2020.

KAZI

Nafasi ya kazi Head of Departiment, Tuma maombi kabla ya tarehe 16 September 2016

NAFASI YA KAZI HEAD OF OPERATIONS
PRESIDENTAL TRUST FUND FOR SELF RELINCE
Is a financial institution, established by the government of Tanzania in 1984 under the Trustees incorporations ordinance chapter 375
The objective of PTF is to promote self help and self- employment spirit to marginalize especially to empower youth and women in Tanzania by providing innovative financial and non financial through a team of competent staff in ensuring creation to the beneficiaries
President Trust Fund invites competent enteric self motivated for the below analyzed and seek to appoint dedicated highly organized and qualified candidates for the following options
1. HEAD OF OPERATIONS
QUALIFICATONS AD SPECIFICATIONS
-          degree in banking accountancy, economics or business administration’s from recognized institute
-          master degree in business administration re added advantage
-          having trained in the knowledge and clear understanding of procurement regulations policies and laws governing the microfinance sector
-          familiar with computer and banking applications
-          customer satisfaction orient ant and sales competencies
-          ability to work in goal and oriented environment
Duties
-          to manage credit portfolio
-          to coordinate and organize the operations
-          to maintain consistence and protect the portfolio from fraud

2. INTERNAL AUDIT
QUALIFICATIONS
-          graduate in accountancy from recognized institutions and holder of CPA or its equivalent qualifications
-          registered with NBAA in the category of certified public accountant
-          at least 5 yrs experience in an accountant/auditor
main duties
-          to perform and control the full audit cycle including risk management control management over operations effectiveness, financial reliability compliance with all applicable directives and regulations
-          to formulate and recommend short and medium term plans of the internal audit-sections
-          to send continuously evaluate departments performance with the aim of maintaining high standard and keep the staff morale high
-          asses the degree of ad hence to fund polices and regulations by the different department
PROCUREMENT OFFICER
QUALIFICATIONS
-          Bachelor degree in procurement
-          Registered with procurement and supplies professionals technician board

MAIN DUTIES
-          To development PTF procurement strategy
-          Creation and mange short mid and long goals and objectives
-          Liaise with PTF’s service providers
-          management of procurement during sourcing contracting suppliers management and support PTF internal procurement activities
Send your application to
CHIEF EXECUTIVE OFFICER
PRESIDENTIAL TRUST FUND FOR SELF RELIANCE
P.O. BOX 70000
DAR ES SALAAM
DEADLINE IS 16th September 2016

AKUTWA KAFARIKI

Akutwa Amefariki Chumbani kwake

mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Patrick Samson maarufu kwa jina la Nchumila,mkazi wa Kata ya Nyihogo wilayani Kahama mkoani aliyekutwa ndani akiwa amefariki dunia baada ya mwili wake kukaa ndani ya chumba na kuanza kutoa harufu Kali iliyosikika kwa majirani zake.

Akidhibitisha kutokea kwa tukio hil o Afisa mtendaji wa mtaa wa Sazia Simon Mabumba amesema alipokea taarifa majira ya saa tisa arasiri kutoka kwa majirani zake na hivyo kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi wilayani hapa ambao kutokana na mwili kuharibika vibaya waliruhusu shughuli za maziko ziendelee.

Hata hivyo kwa mujibu wa Afisa Mtendaji huyo chanzo cha tukio la kifo cha mtu huyo hakijafahamika kutokana na marehemu huyo alikuwa na tatizo la akilili na siku ya mwisho marehemu alionekana akiwa amelewa.

Kwa upande wake mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambae hakutaka jina lake litajwe mtandaoni amesama kuwa ametoa msaada wa kutoa taarifa hiyo katika vyombo vinavyo husika baada ya kukuta harufu kali imetanda kwenye eneo hilo wakati alipofika kwa lengo la kumsalimia mama yake.


VIONGOZI CHAUMA

Viongozi Chaumma waungana na JPM kuhamia Dodoma

Dodoma. Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) kimempongeza Rais John Magufuli kwa hatua yake ya kutekeleza azimio la kuhamishia makao makuu ya Serikali mkoani Dodoma, huku kikisema huo ndiyo ulikuwa mkakati wa chama hicho wa muda mrefu.

Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Kayumbo Katubali alisema ujio wa Serikali bado ni wa kusuasua kuliko kama Chaumma kingeingia madarakani kwani kilikuwa na mkakati thabiti wa kuanzia Serikali yao Dodoma tangu siku ya kiapo.

“Nampongeza Magufuli, ametuonyesha kwa vitendo siyo maneno yaliyokuwa yakisemwa na wanachama wa chama chake kwa zaidi ya miaka 40. Sisi kwenye ilani yetu ya Uchaguzi Mkuu tulipanga kuanzia Dodoma na si vinginevyo,” alisema Kabutali.

Kabutali alisema kwenye ilani yao ya uchaguzi, ibara ya 18 walieleza Serikali yao itakuwa Dodoma baada ya kutangazwa washindi. Mwanasiasa huyo alimtaka Rais Magufuli kukamilisha mchakato wa kuhamia mjini hapa kwa kuutungia sheria ili wanasiasa wasitoe matamko yasiyo na tija.

Kuhusu wakazi wa Dodoma alisema kuwa huenda ikawa faraja kwao kwani kwa sasa Serikali itakuwa karibu nao hivyo watapumzika manyanyaso waliyokuwa wakiyaopata wanapotafuta ardhi.

Alisema wakazi wa Dodoma walishachoshwa na urasimu wa Mamlaka ya Uendelezaji Makao Makuu (CDA) na ndiyo maana migogoro ya ardhi ikawa haimaliziki. Aliwataka wana-Dodoma wawe makini na wasikubali kudanganywa na wajanja katika masuala ya ardhi.

KUTOKA KARAGWE

Karagwe: Walimu watatu wasimamishwa kazi kwa tuhuma ya mapenzi

Karagwe. Mkuu wa Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, Godfrey Mheluka amewasimamisha kazi walimu watatu wa Shule ya Sekondari Kituntu kwa madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi shuleni hapo.

Pia, ameunda kamati kuchunguza tukio hilo ambayo ameipa siku 14 ikamilishe kazi hiyo.

Akitoa agizo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule hiyo, Mheluka alisema zipo taarifa nyingi zinazoripotiwa kwenye ofisi yake kuhusiana na vitendo hivyo.

Alisema ili kudhibiti hali hiyo, ameamua kuwasimamisha kazi walimu hao kupisha uchunguzi.

“Hatuwezi kukubali kuona mwanafunzi anageuzwa mke wakati mzazi kajinyima na kumhudumia mwanaye ili asome kwa ajili ya manufaa yake ya baadaye, na ikibainika kweli wanafanya vitendo hivyo, hatua za kisheria dhidi yao zitachukuliwa,” alisema Mheluka.

Hata hivyo, miongoni mwa walimu waliotajwa, Deodatus Lusatu alikanusha kuhusika na vitendo hivyo huku akidai kuwa anafanyiwa hila na watu wenye nia mbaya na yeye.

Alimpongeza mkuu wa wilaya kwa kuunda kamati ya uchunguzi, huku akitaka watu wote wenye ushahidi dhidi yake, wajitokeze mbele ya kamati hiyo ili ukweli ufahamike badala ya kuendelea kumpaka matope.

“Siwezi kufanya matendo ya kishetani kama haya, nina akili timami na kama ninafanya vitendo hivyo sipaswa kuendelea kuwapo chini ya jua,” alisema Lusatu.

Mkuu wa Wilaya Mheluka alisema utaratibu wote wa kiutumishi utafuatwa bila kumuonea.

Katibu wa Tume ya Nidhamu na Maadili ya Walimu (TSD) Wilaya ya Karagwe, Fredrick Kabendwe alisema, atafanya kazi sanjari na kamati atakayoiunda ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo.

Mkazi mmoja wa wilaya hiyo, Sadiki Juma alisema tuhuma hizo zinapaswa kuchunguzwa kwa makini kwani zinaweza kuwa ni chuki binafsi.

Katika hatua nyingine, Mheluka aliwataka wazazi, walezi na wananchi wa wilayani Karagwe kutoa ushirikiano kwa Serikali ili kuiwezesha sekta ya elimu kufikia malengo wanayokusudia.

Pia, aliwataka kutunza na kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti na kuacha kutochoma moto ovyo, yeyote atakayebainika sheria itachukua mkondo wake.

video with beyonce

Video: Beyonce asababisha Rapper wa Marekani kuvunja mahojiano baada ya kumgusa

Hata ukiwa unajiona wewe ni muongeaji sana lakini siyo pale utakapokutana na Beyonce – unaweza ukageuka bubu kwa muda.

Kilichomtokea rapper wa Chicago, Chance the Rapper wikiendi hii kwenye backstage ya tuzo za MTV VMA lazima atakiweka kwenye kumbukumbu ya maisha yake kwa kuwa watu wengi wanatamani kiwatokee.

Wakati Chance the Rapper akihojiwa na mtangazaji wa MTV, Meredith Graves kuna mtu alikuja nyuma ya rapper huyo na kumlalia kwenye upande wa bega lake la kushoto alipogeuka alishangaa kumuona ni Beyonce aliyefanya kitendo hicho.

Ilikuwa ni kama ndoto kwa rapper huyo alijikuta akimkumbatia malkia huyo na kushindwa kumwambia chochote na hata interview ikaishia hapo huku akimalizia kwa kusema “This is my life.”

Hata Dj Khaled aliwahi kuliambia gazeti la The New York Times kuwa heshima aliyonayo kwa Bey ni kubwa mno kiasi cha kuwa muoga wa kuongea sana akiwa naye ili asije akaharibu.

Queen Bey aliongoza kwa kuchukuwa tuzo nane katika vipengele 11 alivyokuwa amewekwa kwenye tuzo hizo.