There was an error in this gadget
SUNDAY, AUGUST 07, 2016
RAIS DKT. MAGUFULI ASALI KATIKA KANISA LA BIKIRA MARIA PAROKIA YA CHATO, PIA ATEMBELEA KANISA LA ANGLIKANA, AIC PAMOJA NA MSIKITI WA OMAR BIN-L-KHATTAB CHATO MKOANI GEITA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakisali katika ibada ya Jumapili katika Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waamini wa kanisa Katoliki wa Parokia ya Chato mara baada ya Ibada katika kanisa hilo Chato Mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihamasisha mchango wa ujenzi wa Kanisa jipya la la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
SUNDAY, AUGUST 07, 2016 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG HABARI, IBADA, RAIS MAGUFULI ~MTUMIE RAFIKI YAKO , MAONI: 0
SUNDAY, AUGUST 07, 2016
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWASILI MKOANI LINDI TAYARI KWA MAADHIMISHO YA KILELE CHA SIKU YA WAKULIMA NANENANE KESHO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Lindi mchana huu akitokea mkoa wa Dar es Salaam kwa njia ya barabara ambapo hapo kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane kitaifa kwenye viwanja wa Ngongo katika Manispaa ya Lindi.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufunga maonyesho hayo ya Nane nane hapo kesho kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli.
Alipowasili ikulu ndogo mjini Lindi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Mkuu wa mkoa wa LINDI Godfrey Zambi pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali na wa vyama vya siasa.
Katika Msafara wake, Makamu wa Rais ameambatana na Waziri wa Kilimo, Maliasili na Uvuvi wa Zanzibar Mhe. Hamad Rashid.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mstahiki Meya wa Lindi mjini Ndugu Mohamed Liumbwe mara baada ya kuwasili mkoani Lindi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivishwa skafu wakati wa mapokezi na Vijana wa mkoa wa Lindi .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Wakina Mama wa mkoa wa Lindi wakimuimbia nyimbo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa mapokezi mkoani hapo.
Wakina Mama wa mkoa wa Lindi wakimuimbia nyimbo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa mapokezi mkoani hapo.
SUNDAY, AUGUST 07, 2016
WAZIRI MKUU MAJALIWA USO KWA USO NA ASKOFU GWAJIMA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Uzima na Ufufuo katika hafla ya harusi ya Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Amon Mpanju na mkewe Analises iliyofanyiak kwenye ukumbi wa jeshi wa Lugalo jijini Dar es salaam Agosti 6, 2016.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Amon Mpanju akilishwa keki na mkewe , Analises katika tafrija ya harusi yao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam Agosti 6, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary walihudhuria katika tafrija hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Amon Mpanju akimlisha keki mkewe , Analises katika tafrija ya harusi yao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam Agosti 6, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary Walihudhuria katika tafrija hiyo.
SUNDAY, AUGUST 07, 2016
WAKAZI WA MBEYA WANUFAIKA NA GULIO LA SIMU LA BEI CHEE ZA VODACOM TANZANIA
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania, Lawreny Vimenty(kulia) akimkabidhi John Mwalusako simu aliyonunua jana katika Gulio la simu linaendeshwa na kampuni hiyo, katika kituo cha mabasi cha nane nane wakati wa maadhimisho ya wakulima Nane nane yanayoendelea katika uwanja John Mwakangale jijini Mbeya.
Wacheza shoo wakiendelea kutoa burudani kwa wateja waliofika kwenye Gulio la simu lililoendeshwa na Vodacom Tanzania,katika kituo cha mabasi cha nane nane wakati wa maadhimisho ya wakulima Nane nane yanayoendelea katika uwanja John Mwakangale jijini Mbeya.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania(wenye flana nyeusi) wakitoa huduma mbalimbali kwa wateja waliofurika katika Gulio la simu liloandaliwa na kampuni hiyo,katika kituo cha mabasi cha Nane nane nje ya viwanja vya maonyesho ya wakulima Nane nane maarufu John Mwakangale.
SUNDAY, AUGUST 07, 2016
BWAWA LA MAINI LILIVYOITANDIKA BILA HURUMA TIMU YA DUNIA MABAO 4-0 KATIKA DIMBA LA WEMBLEY
Ulikuwa usiku mujarabu kwa vijana wa Jurgen Klopp, Liverpool ndani ya dimba la Taifa la Ungereza,Wembley baada ya kuisambaratisha bila huruma bingwa wa Laliga Barcelona kwa mabao 4-0 na kuwaacha mashabiki wengi wa soka Ulimwenguni wasiamini walichokiona na kukisikia.
Wakicheza kwa kujituma huku wakifahamu wazi kuwa wanacheza na timu bora kabisa duniani, wachezaji wa Liverpool walihakikisha hawawapi nafasi wapinzani wao kumiliki mpira kwa kuingilia pasi zao,dakika ya 14, Lalana anamnyang'anya mpira Alex Vidal na kumpa pasi Firmino ambaye anamrudishia Lalana naye anampa tena Sadio Mane na bila ajizi anaukwamisha mpira huo wavuni,1-0.
Goli hilo linadumu hadi mapumziko, kipinndi cha pili kilipoanza inachukuwa dakika moja tu Liverpool wanaandika bao la pili kwa beki Mascherano kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa mpira uliopigwa na Sadio Mane.
Dakika moja baadaye yaani dakika ya 47, Stewart anampokonya mpira Busquets na kumpenyezea pasi murua Diovick Origi anayewazidi mbio Gerard Pique na Mascherano nakupiga shuti linalopita katikati ya miguu (tobo) ya kipa wa Barcelona Terstegen. 3-0.
Katika kipindi hiki timu zote zilifanya mabadiliko ya wachezaji zaidi ya 6 kwa kila timu, na hapo Barcelona walitawala zaidi mpira na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Liverpool lakini ngome ya Liverpool ambayo iliongozwa na Lovren ilicheza kwa nidhamu ya hali ya juu na kufanikiwa kuzuia hatari zote.
Watu wakiamini kuwa mchezo unamalizika kwa hayo mabao matatu, Dakika ya 92 yaani dakika moja kabla ya mpira kumalizika kwa zile dakika za nyongeza Liverpool wanapora mpira katikati ya uwanja na kufanya shambulizi la kushitukiza, ambapo mpira wa krosi unapigwa na Markovic unatua kichwani kwa Grujic na kuupiga pembeni juu ya kona ya goli, waswahili hupenda kuita "anapotagia ndege" na mpira huo kutinga wavuni na kuandika bao la nne, hivyo kuhitimisha karamu hiyo ya mabao.4-0.
SUNDAY, AUGUST 07, 2016
MASHINDANO YA MAJESHI KUFUNGULIWA RASMI KESHO NCHINI RWANDA, JWTZ WAWASILI SALAMA MJINI KIGALI
Na Selemani Semunyu, JWTZ
Timu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzani limewasili Salama katika Mji wa Kigali Nchini Rwanda kuungana na Wanajeshi wa Nchi Za Afrika Masahariki katika Mashindano ya majeshi kwa nchi hizo yanayotajiwa kufunguliwa Rasmi kesho.
Kiongozi wa Msafara wa Timu hiyo Brigedia Jenerali Jairos Mwaseba Alisema muda mfupi baada ya Timu hiyo kuwasili kuwa Timu iko salama na Wameanza mazoezi mepesi kwa Ajili ya Kujiandaa na Michuano hiyo sambamba na kuzoea hali ya hewa.
“Timun yetu iko vizuri kilizhobaki watanzania waendelee kuiombea Timu yetu kwani maombi yao yakichanganyika na jitihada za Timu basi ushindi utapatikana na ni vema Watanzania walioko Rwanda kujitokeza kushangilia Timu zao,Alisema Brigedia Jenerali mwaseba.
Wakati huo huo Mkuu wa majeshi wa Rwanda Jenerali Patrick Nyamvumba akizungumza Na Waandishi wa Habari alisema Maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa ni kuanza kwa Michezo hiyo huku Timu zikimalizia hatua za Mwisho za Usajili kwa ajili ya Michuano hiyo
Alisema Wanajeshi 500 kutoka katika Majeshi ya Nchi Nne za Tanzania,Rwanda,Uganda, na Kenya wanatarajiwa kushiriiki katika Mashindano ya Kumi ya Majeshi ya Nchi za Afrika Mashariki huku Burundi ikiwa imeshindwa kushiriki kutokana na hali ilivyo katika Nchi yake.
Jenerali Nyamvumba alisema anamatumani makubwa na mazungumzo yanayoendelea kuhusu Burundi hivyo Matarajio yake yataifikisha Burundi katika Hatua Nzuri na Hivyo kushiriki katika Michezo hiyo ambayo aliita Muhumi kwa Ushirikiano.
“Michezo hii ni Muhimu kwa Ushirikiano wetu kwani hakuna Mshindi mwisho wa mashindano sote tunakuwa washindi kutokan na kufanikisha kuwa pamoja,Urafiki kama kamajeshi yaliyo katika Ukanda wa Afrika Mashariki,” Alisema Jenerali Nyamvumba.
Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi kutoka Tanzania Brigedia Jenerali Martin Kemwanga amesema kama kamati waliridhia kuwepo kwa Michezo Mitano ambayo ni Mpira wa miguu,Kikapu,Pete,Mikono na Mbio za Nyika.
Mkuu wa Majeshi ya Rwanda (CDS) Jenerali Patrick Nyamvumba (Kushoto)akiongea na Waandishi habari Hawapo Pichani katika Ukumbi wa Uwanja wa Amahoro Juu ya maandalizi ya mashindano ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki yanayotarajia kufungulia Kesho(Leo Jumatatu Agosti 8)Kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Mandalizi Brigedia Jenerali martin Kemwanga wa JWTZ.
Mwenyekiti wa kamati ya Mandalizi ya Mashindano ya 10 ya Majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki Brigedia Jenerali Martin Kemwanga wa JWTZ akifafanua jambo Mbele ya Waandishi wa habari (Hawapo Pichani)Mjini Kigali kuhusu Maandalizi ya mashindano hayo kushoto ni Mkuu wa Majeshi wa Rwanda (CDS) Jenerali Patrick Nyamvuba ).
Baadhi ya Viongozi na Wachezaji wa Timu za Jeshi wanaoshikiri Michuano ya Kumi ya Majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki yanayotaraji kufunguliwa Kesho (Leo) katika Uwanja Wa Amahoro Mara walipowasili katika Mji wa KigalI Nchini Rwanda .(Picha na Selemani Semunyu).












No comments:
Post a Comment