Gadget
| This content isn't available over encrypted connections yet. |
SATURDAY, AUGUST 20, 2016
JK AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KWENYE MAZISHI YA BI SHAKILA MBAGALA CHARAMBE JIJINI DAR.
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Bi Shakila Said,wakati wa maziko huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2016.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye akiweka udongo kwenye kaburi la Bi Shakila Said,wakati wa maziko huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar.
Rais Mstaafu awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo cha Bi Shakila Said ,huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar,wa pili kushoto aakishuhudia ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye na Katibu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw. John Kitime.
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiweka saini kitabu cha maombolezo cha Bi Shakila Mbagala Charambe,jijini Dar es salaam. Kushoto ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye.
Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo cha Bi Shakila Said huko nyumbani kwa marehemu Mbagala Charambe,jijini Dar es salaam.
Rais Mstaafu awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete (wa pili kulia) na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye (pili kushoto) wakishiriki maziko ya aliyekuwa Mkongwe,mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarabu hapa nchini,Bi Shakila Saidi ambaye mazishi yake yamefanyika leo huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar.
SATURDAY, AUGUST 20, 2016
JESHI LA POLISI LAPIGA MATIZI YA UTAYARI WA KUKABILIANA NA MATUKIO YA UHALIFU NA WAHALIFU NCHINI
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wa wakiwa moja ya maozezi yao ya kupasha viungo kabla ya kuanza mazoezi ya kutuliza ghasia.
Askari Polisi wa kikosi maalum cha polisi (CRT) wa mkoa wa Iringa wakiwa katika mazoezi ya utayari wa kukabiliana na matukio yoyote yatakayojitokeza katika maeneo mbalimbali.
Askari wa vikosi vya kutuliza ghasia wa mikoa mbalimbali wakiwa na magari yao wakati wa mazoezi ya utayari wa kupambana na matukio mbalimbali ya uhalifu na wahalifu katika maeneo mbalimbali.
Askari wa vikosi vya kutuliza ghasia wa wakiwa na magari yao wakati wa mazoezi ya utayari wa kutuliza ghasia na kukabiliana na matukio yoyote ya uhalifu na wahalifu.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI




No comments:
Post a Comment